Page Nav

HIDE

Breaking News:

latest

Ads Place

Je Vipi Kuhusu Siagi ya Karanga?

Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa nakiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa...

Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa nakiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu,hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.
Siagi ya karanga ina kiasi kingi cha mafuta masafi yasiyoweza kusababishakolesto/lehemu mwilini (unsaturated fats) na kiasi kingi cha protini, vitu hiviviwili vinafanya kazi ya kuongeza nguvu mwilini. Siagi ya karanga ina kalorinyingi zitakazokuwezesha ubaki ni mwenye nguvu kutwa nzima.
Kwakuwa ni chanzo kizuri cha madini ya chuma, shaba, magnesium, na potasiamu,siagi ya karanga ni nzuri sana katika kuuweka katika usawa mzuri mzunguko wadamu mwilini.
Kadharika kiasi kingi cha protini kilichomo kwenye siagi ya karanga kinasadikikakuwa na uwezo wa kuongeza nguvu au uwezo wa mwili na kutengeneza mishipa mingina imara zaidi.
Kaanga kidogo karanga bila kuziunguza na usizitie chumvi, kisha zimenye auondoa maganda yake. Saga kwenye blenda huku ukiongeza kidogo kidogo mafuta yoyoteya mboga mboga kama ya alizeti au mafuta ya karanga, ongeza sukari au asalikidogo na chumvi kidogo.
Mimi napenda zaidi kuitumia kwenye mkate lakini pia unaweza kuongeza siagi yakaranga kwenye karibu kila mboga ya majani, samaki na kadharika. Ukiacha radhayake nzuri na tamu, siagi ya karanga ni chakula chenye afya na nguvu nyingi naisiyo na takataka zozote zisizohitajika na mwili.

No comments

Latest Articles